Southgate awataka wachezaji wake kupambana hadi tone la mwisho la damu dhidi ya Colombia

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amewataka wachezaji wake kupamabana hadi tone la mwisho la damu yao wakati watakapo wakabili Colombia hii leo kwenye mchezo wa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi.

Uingereza ambayo imeingia hatua ya 16 bora itakuwa na kibarua kizito dhidi ya timu ya taifa ya Colombia ili kujihakikishia inasonga mbele hatua ya robo fainali kisha kukutana na mshindi kati ya Switzerland au Sweden.

Nadhani maisha siku zote ni kupata nafasi na kuhakikisha unaidhibiti, tumesema kamwe hatuwezi kuwa kwenye haya mashindano na kuondoka.

Sote ni lazima tupambane hadi mwisho wetu na nilazima tushinde huu mchezo, maandalazi yetu yamekwenda vizuri na kwa sasa nilazima tuache maneno mengi na tupate kile tulichopanda.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW