Habari

Spika ashangazwa na shangwe za wabunge kwa Kikwete

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameshangazwa na jinsi wabunge walivyomshangilia Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na kuelezea kuwa hakuna mgeni aliyewahi kupata shangwe kama hizo.

Rais Mstaafu huyo ameshangiliwa kwa muda mrefu mara baada ya kuingia bungeni leo asubuhi alipoenda kumshuhudia mke wake, Mama Salma akiapishwa tangu ateuliwe kuwa mbunge.

“Waheshimiwa wabunge, binafsi mimi ni kipindi cha nne humu bungeni sijawahi kuona mgeni amepokelewa kwa kiwango hiki,” alisema Spiga Ndugai huku akicheka kwa furaha.

Ikumbukwe kuwa Bunge limeanza leo mjini Dodoma.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents