Habari

Spika Job Ndugai apongezwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushiriki kikamilifu kampeni ya Wabunge katika zoezi la upimaji Ukimwi kwa hiari.

Waziri Mkuu amepotoa Pongezi hizo leo, Juni 29, 2018 Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa jambo la upimaji ni muhimu kwao viongozi.

“Nitumie fursa hii kukupongeza wewe binafsi Mh. Spika kwa kushiriki kikamilifu katika kampeni ya upimaji na kuongoza Waheshimiwa Wabunge katika upimaji wa hiari tarehe 21 Juni, 2018. Jambo hili ni muhimu kwetu sisi viongozi. Aidha, kufuatia zoezi hilo, wale watakaogundulika wana maambukizo ya VVU, ninawasihi waanze mara moja kutumia dawa za kufubaza. Waheshimiwa Wabunge, nasi pia katika majukwaa yetu ya kisiasa tuendelee kuunga mkono kaulimbiu ya “FURAHA YANGU – PIMA, JITAMBUE, ISHI” ili Watanzania wajitokeze kwa wingi kupima afya zao popote pale walipo,” alisema Waziri Mkuu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents