Habari

Spika Ndugai afunguka hili kuhusu kuwataja Mawaziri na Wabunge wenye mahudhurio hafifu bungeni

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema lengo la kuwataja Mawaziri na Wabunge ambao wana mahudhurio hafifu ndani ya Bunge haikuwa kuwachongea kwa viongozi wa vyama vyao bali ni kuwataka kutimiza wajibu wao wa kuingia bungeni.

Kwa mujibu wa Spika Ndugai Mawaziri wengi wanashindwa kuhudhuria bungeni, kwa kisingizio cha  kuwa wako kwenye maeneo mbalimbali wanatatua changamoto za wananchi wakati wawakilishi wao wako bungeni.

Akizungumza na www.eatv.tv Spika Ndugai amesema “Nia haikuwa kumchongea mbunge yeyote, kumbuka hata mawaziri nao wanakuwa wabunge kabla ya kuwa mawaziri, na uzuri wa bunge letu linaratiba ya mwaka mzima, wanapokuja pale wanakuja na ratiba nchi nzima, haiwezekani mimi mbunge wa Kongwa bunge linaendelea halafu Waziri anaenda Kongwa.

Kwa sasa siwezi kuwataja tena, orodha ya wabunge ambao ni watoro ila kwa faida ya wananchi tutawatajia mwishoni ili inapofika kipindi cha uchaguzi, watambue ni mbunge gani ambaye walimuagiza bungeni lakini alikuwa ahudhurii, amesema Spika Ndugai

Mfano huyo Mbunge wa Arusha Mjini (Godbless Lema,) kutwa yuko kwenye mitandao ya kijamii anadhani ubunge ni mtandaoni, na hata hao mawaziri niliwaambia wawajibu wapinzani kwenye mitandao ya kijamii sikumaanisha wasije bungeni wanatakiwa pia wafike bungeni.

Wiki iliyopita wakati wa Mkutano 13 wa Bunge Spika Job Ndugai aliwataja orodha ya wabunge na Mawaziri ambao ni watoro bungeni akiwemo Waziri Januari Makamba, Palamagamba Kabudi, na kwa wabunge alimtaja Godbless Lema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents