Habari

Spika Ndugai apima UKIMWI kuhamasisha Wabunge (+Picha)

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo amezindua maonyesho ya zoezi la kupima Ukimwi kwa Wabunge kwa hiari lililofanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Maonyesho hayo yameandaliwa na Taasisi za Kijamii zinazotoa huduma na Mwitikio wa Ukimwi.


Spika wa Bunge,Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Oscar Mukasa katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Kabla ya Mhe. Ndugai kuwaongoza Waheshimiwa Wabunge katika upimaji wa Virusi vya Ukimwi (VVU)

Tazama Picha zaidi:


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akiongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Iringa, Mhe. Rose Tweve wakielekea katika Upimaji wa Virusi vya Ukimwi (VVU) na kwenye Maonyesho yaliyoandaliwa na Taasisi za kijamii zinazotoa huduma za mwitikio wa UKIMWI yaliyofanyika leo tarehe 21 Juni, 2018 katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma


pika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipima Virusi vya Ukimwi na kuhamasisha Waheshimiwa Wabunge Upimaji wa Virusi vya Ukimwi (VVU) leo tarehe 21Juni, 2018 katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipatiwa maelezo na Mratibu wa Baraza la watu Wanaoishi na Virusi vua Ukimwi Tanzania (NACOPHA) kanda ya Dar es Salaam, Ndg. Edna Edson katika Maonyesho ya Taasisi za kijamii zinazotoa huduma za mwitikio wa UKIMWI yaliyofanyika leo tarehe 21 Juni, 2018 katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Taarifa na Mipango kutoka Taasisi ya Utawala na Maendeleo ya Afya (MDH), Dkt. Lameck Machumi katika Maonyesho ya Taasisi za kijamii zinazotoa huduma za mwitikio wa UKIMWI yaliyofanyika leo tarehe 21 Juni, 2018 katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma

Picha na Ofisi Ya Bunge

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents