Habari

Spika Ndugai athibitisha hili kuhusu matibabu ya Mh. Lissu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema utaratibu unaofanywa na serikali nikuangalia namna gani watatakiwa kugharamia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyepigwa risasi Septemba 7 mwaka 2017 mjini Dodoma na watu wasiojulikana.

Spika Ndugai akizungumza na Azam News baada ya familia ya Lissu kulalamika kuwa pamoja na kuandika barua kwa ofisi ya Bunge hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

“Suala lake kidogo ni tofauti ni kweli kwamba atapelekwa nje zaidi ya Nairobi bado mpaka sasa sijui ni lini atapelekwa nje sina tarehe bado, lakini nadhani itakuwa ni hivi karibuni na wale wanaogharamia kumpeleka nje washawasiliana na mimi,” alisema Spika Ndugai.

“Naamini hakika hata familia ya Lissu na Lissu mwenyewe hatakuwa hajui hilo anafikiri ni wao wenyewe lakini najua na walishafika kwangu wakasema watagharamia hilo na watakavyofanya hivyo gharama ambAzo sisi tunaweza tukaziingilia ni zile zilobakia, na hivyo tunatakiwa kujua kuwa vitu gani tunalipia na hatutakiwi kulipia kwasababu tukisema tulipe bila mpangilio utakuwa ni mkanganyiko usio na afya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents