Moto Hauzimwi

Spika Ndugai atishia kumpiga ‘stop’ mbugeni Zitto Kabwe hadi 2020

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amezidi kumuonya mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa kauli zake za kudhalilisha Mhimili wa Bunge na kumwambia kuwa anao uwezo wa kumzuia kutozungumza Bungeni chochote miaka yote ya Bunge.

Zitto Kabwe

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe hawezi na hapaswi kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha na aliyekuwa Spika wa Bunge marehemu Samuel Sitta.

“Nimwambie Zitto, una uwezo wa kupambana na Spika kweli? Nina uwezo kukupiga marufuku kuongea humo mpaka miaka yako ikaisha, hakuna pakwenda, hakuna cha swali, hakuna cha nyongeza, hakuna cha kuongea chochote humo ndani ya Bunge utanifanya nini. Pambana na kitu kingine na siyo Ndugai”, amesema Spika Ndugai.

Hapo jana Spika Ndugai alimtaka Zitto Kabwe kufika kwenye kamati ya maadili kutoa maelezo juu ya taarifa alizoziweka kwenye mtandao, na Zitto Kabwe kumjibu kuwa mambo anayoyafanya Spika yanaporomosha bunge

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW