Habari

Spika Ndugai auchambua mkutano wa nane wa Bunge

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ameuchambua mkutano wa nane wa Bunge la 11, ikiwemo mivutano iliyojitokeza kati yake na baadhi ya wabunge wa upinzani na kazi za bunge zilizokuwa zikiendelea.

Akizungumza na Azam Tv, Spika Ndugai amesema kuwa yeye hana ugomvi na mbunge, Zitto Kabwe, Kubenea na Godbless Lema ambaye ni mbunge wa Arusha mjini.

“Bunge hili ni la wiki mbili ni la muda mfupi sana kwa kazi za bunge, wabunge wamefanya kazi vizuri wamelichambua kwenye level ya kamati, wamesikiliza maoni ya wadau na imefika hapa bungeni imejadiliwa kwa uwazi ikafanyiwa mabadiliko muhimu yaliyotakiwa kufanyika na baadae ikapitishwa, kwa ujumla wake tunawashukuru wabunge tunashukuru serikali kazi hii imefanywa vizuri kwa niaba ya Watanzania,” alisema Spika Ndugai.

Hata hivyo Spika Ndugai alipoulizwa kuhusu mivutano iliyotokea kati yake na Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe, Said Kubenea, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema ni bora mwandishi akawauliza wahusika wenyewe, huku akisema kuwa yeye hana ugomvi na wabunge hao huku akisema walipokuwa wakifanya kazi za hapo bungeni wao hawakuwepo bungeni Dodoma walikuwa katika maeneo wanayoyajua wao, pia amekuwa akiwashangaa wabunge hao wakitumia mitandao na kujirokodi kuzungumza mambo mbalimbali ambao hayana mantiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents