Habari

Spika Ndugai aunda tume ya wajumbe 9

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameunda Kamati Maalumu ya wajunge tisa (wabunge) itakayochunguza suala la uchimbaji wa Madini ya Almasi hapa nchini ambayo itafanya kazi  ndani ya siku 30.

Spika Ndugai ametoa orodha ya Wabunge hao leo bungeni mjini Dodoma wakati wa kuhairishwa kwa Bunge.

“Naomba nitoe ufafanuzi wa kuunda Kamati Maalum itakayo tathimini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki, udhibiti wa Madini ya Almasi kisha kuandaa mapendekezo mahususi kwaajili ya kuishauri serikali kuhusiana na uendeshaji bora wa biashara ya Madini ya Almasi nchini, Chimbuko la jambo hili ni tarehe 15 Juni nilipohudhuria pale Ikulu kwa niaba yenu waheshimiwa wabunge wakati wa ripoti ya pili na Profesa Nehemia Oroso ambayo ilikuwa inaangalia masuala ya kiuchumi na kisheria kuhusu usafirishaji wa Makinikia ilipotolewa pale na mimi niliahidi kwamba tutaangalia kwenye eneo lenye Madini ya Almasi,” alisema Spika Ndugai.

“Kwa hatua hii mkumbuke tumeshaunda Kamati ya kuangalia Madini ya Tanzanite hapo kabla lakinin pili kufanya hivi ni malalamiko ya wananchi ikiwa ni pamoja na Kamati ya Nishati na Madini ambayo pia imekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kuhusiana na eneo hili nimeunda kamati maalumu ya ushauri, nimeteua wajumbe Tisa (Wabunge) na kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa siku 30 na kituo kikuu cha kazi zao kitakuwa hapa bungeni mjini Dodoma itakapo bidi kamati itaweza kufanya ziara popote pale nchini itakapo bidi na Mwenyekiti wa kamati hii atakuwa Mussa Azzan.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents