Habari

Spika Ndugai azuia hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani isisomwe Bungeni

Spika wa Bunge, Job Ndugai amezuia kusomwa kwa hotuba ya Kambi ya upinzani Bungeni na akidai kuwa imejaa makosa takriban kila ukurasa, ina matumizi mabaya sana ya jina la Rais Magufuli na kulituhumu Bunge la 11.

Amesema “Kulifanya Bunge kuwa mahala pa uzushi haifai, kwa hiyo kwa mamlaka niliyonayo, sitaruhusu hotuba ya Kambi ya Upinzani kusomwa Bungeni kwasababu inavunja kanuni kadhaa. Na hotuba zinazokuja huko mbele zikiwa za aina hii itakuwa hivyo hivyo”

Amesema awali alikuwa akiwaonya Kambi hiyo kwa kuwataka kuondoa baadhi ya maeneo katika hotuba zao yanayokwenda kinyume na kanuni lakini kuanzia sasa atakuwa hafanyi hivyo na badala yake ataondoa hotuba nzima yenye maeneo yanayokiuka kanuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents