Habari

Sporah Show: Mr Blue alidate wasichana 3 wakati mmoja na wao wakifahamiana, Wahida, Naj na mwingine kwa zaidi ya miaka 7 (Video)

Mr Blue was a qualified play boy. Hivi karibuni kwenye kipindi cha TV cha The Sporah Show alifunguka kwa urefu masuala mengi ambayo yalikuwa hayajulikani kuhusu uhusiano wake na Naj pamoja na mama wa mtoto wake, Wahida.

http://www.youtube.com/watch?v=5bgHaYFvyzI

“Kiukweli kulikuwa na wasichana watatu, Naj na msichana mwingine hajulikani hapo na Wahida. Sasa ilivyotokea ile mimba kabla ya marehemu mama yangu hajafa akaniambia ‘bwana inabidi utulie uchague msichana unayeweza kutulia naye’. Kwahiyo nikamwambia ‘huyu msichana (Wahida) mimi nampenda natulia naye na hii mimba na kila kitu. So kuanzia pale mimi nikakata mambo ya kina Naj sijui. Kiukweli hajanikosea chochote,” alisema Blue.

Alisema kuwa alikuwa na wasichana hao watatu kwa wakati mmoja na wote walikuwa wakifahamiana.

“Yaani kama kifalme hivi. Mimi mwenyewe nilikuwa nimechanganyikiwa sijui niwe na nani. Hao watatu ndio nilikuwa napumzika nao vizuri yaani,” alisisitiza.

“Ilifika wakati nikaona nacheza michezo ambayo haina maana.”

Akielezea kwanini aliamua kumchagua Wahida badala ya Naj na huyo msichana mwingine, Blue alisema, “ametulia, nampenda, ananisikiliza. Halafu kingine Naj kuna distance pale ilikuwa, yeye yuko huku (Uingereza) mimi nipo Bongo, kuna kauongo kanaendelea.

Unajua ilitokea gazeti moja linaitwa Babkubwa lipo Bongo, Naj alikuja tukapiga picha, zile picha zikawekwa kwenye front page kabisa. Kwahiyo ibadi ugomvi ukawa mkubwa sababu yule (Wahida) alikuwa na ujauzito pale.”

Blue anasema ndio maana aliamua kuwaambia ukweli Naj na huyo msichana mwingine ambaye hakutaja jina lake kuwa ameamua kutulia na Wahida japo anasema haukuwa uamuzi rahisi kwake na kwao pia.

“Ilikuwa kama vita kwakweli halafu wote nimekaa nao muda mrefu, Naj karibu 5 years, yule mwingine karibu seven years, huyu mwingine (Wahida) ndo kazidi 8 years.

“Hakuna aliyekubali kati yao,” alisema Blue kujibu swali la Sporah kwanini asingewaoa wote kwakuwa dini yake inaruhusu.

“Mimi niko tayari, ofcourse naweza nikaoa wake wanne.”

Licha ya kusema kuwa hawezi kuwa tena na Naj, Blue amesema tangazo la show ya Uingereza linalowaonesha yeye na Naj limesabisha ugomvi mkubwa na Wahida ambaye anahisi wapenzi hao wa zamani wanaweza kukumbushia.

“Ilibidi nimwelezee na nini, kwahiyo Naj ni rafiki yangu kwakweli halafu namsupport kwasababu anapenda muziki na nasikia sijui yupo na Diamond, something like that na mimi sijadeal tena na vitu vyake.”

“I did love him, I will always love him,” alisema Naj kujibu swali kama mapenzi yao yalikuwa ya kweli ama kutafuta umaarufu.

“I am not gonna lie, I will always love him. We tried but it wasn’t meant to be, maybe the distance but at the end of the day we are still friends,” aliongeza Naj ambaye amewahi kumshirikisha ex wake huyo kwenye wimbo wake Don’t Let Me Go.

Akijibu jinsi alivyojisikia kuhusu Wahida kuwa mjamzito, Naj alisema: ofcourse like any other girl would be heartbroken, but then when I went into this relationship nilishajua kabisa kwasababu we have to remember it’s a long distance relationship anything can happen kwasababu mimi na yeye tumekutana najua yeye ana maisha gani mimi nina maisha gani but I still accepted that, I mean throughout the whole whatever maybe the trust wasn’t there much hata yeye kwa upande wake, upande wangu it’s always the same but the only thing that kept us coming back to each other was love.”

Naj alisema licha ya ukweli kwamba Blue alikuwa na wapenzi wengine, alikuwa anaona jinsi Kabayser alivyokuwa akimpenda na kumheshimu kwa dhati.

“Yaani huyu (Mr Blue) mapenzi yake, nilikuwa nayaona, when I’m there he treats me like a queen, that’s what I like, respect na nini, wengine nikaona wa kupita tu. He was quite my first love I have to be honest; I have never loved anyone else.”

Hata hivyo Naj alikanusha kuwa aliwahi kuwa na uhusiano na Diamond na kusema kuwa walikuwa marafiki tu.

“Ukweli mimi nilipona huyu Diamond ametoka na huyu (Naj) nilishangaa,” alieleza Kabayser baada ya kuulizwa jinsi alivyojisikia baada kusikia tetesi za Naj na Diamond kuwa pamoja.

“Sikushangaa kwamba huyu (Naj) amekuwa na Diamond sababu huyu tuligombana lazima atakuwa na mwanaume, haijalishi ni Diamond ni nani. Lakini nilijiuza kitu kwa Diamond kwanini anafuatilia watu ambao (nimepitia). At the end of the day nikampigia simu Diamond nikamwambia ebana tunaweza tukaonana, hatukuonana. Nilitaka nimuulize tu hilo swali. Nilitaka nijue kwanini msichana niliyekuwa kuwa naye, huyu wa pili sasa. Diamond mama yake na mama yangu waliwahi kucheza pamoja. Diamond rafiki yangu kabisa, he is my boy lazima nimuulize.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents