MichezoUncategorized

SportPesa kuirudisha Everton kwenye mbio za ubingwa EPL

Klabu ya Everton FC ilianzishwa mnamo mwaka 1878 muda huo ikijulikana kama St Domingo FC huko jijini Liverpool nchini Uingereza kabla ya mwaka 1879 kubadilisha jina na kuitwa Everton baada ya timu mbili za mtaa wa Everton  yaani timu ya kanisa ya Everton Church Club na St Domingo FC kuungana na kuanzisha klabu ya Everton FC.

Tokeo la picha la everton fc sportpesa

Safari ya Klabu ya Everton kuchukua vikombe na mataji ilianza mwaka 1890 baada ya kuchukua kombe la Ligi ya Uingereza mwaka mmoja kabla ya kuanzishwa kwa ligi hiyo mnamo mwaka 1888-89.

Klabu ya Everton ilikaa bila kombe lolote kwa miaka 6 mpaka mwaka 1906 ilipochukua kombe la FA na baadae miaka mingine nane mnamo 1914 kuchukua ndoo ya kombe la ligi ambalo lilikuwa la mwisho baada ya vita ya kwanza na ya pili ya Dunia iliyopelekea michuano yote ya mpira wa miguu kusimama kwa miaka 25 yaani kuanzia mwaka 1914 hadi 1939.

Vita vya pili vya Dunia viliiathiri klabu ya Everton kitu ambacho kilipelekea klabu hiyo kushuka Daraja mwaka 1950-51 jambo ambalo liliwafanya wapambane kurudi tena kwenye Ligi daraja la kwanza hii ni baada ya kushika nafasi ya pili ligi daraja la pili mnamo mwaka 1953-54.

Safari ya Everton haikuwa rahisi kama kusingelikuwa na wachezaji kama Dixie Dean,Neville Southall,Gary Stevens,Brian Labone,Kevin Ratcliffe,Ray Wilson,Trevor Steven (1983–90)Alan Ball,Peter Reid,Kevin Sheedy,Dixie Dean,Graeme Sharp na makocha kama Harry Catterick na Howard Kendall kwani mpaka kufikia mwaka 1992 klabu hiyo ilikuwa tayari imebeba zaidi ya mataji 20.

Klabu ya Everton ambayo maarufu kwa jina la The Toffees ni moja kati ya klabu 20 zilizoingia kwenye Ligi kuu ya England (EPL) mnamo mwaka 1992 ilipoanzishwa rasmi.

Huwezi kuitaja Everton ukaimaliza kama utasahau kutaja uwanja wao Goodison Park ambao mashabiki wao huuta jina la utani la The Grand Old lady kwani katika rekodi uwanja huo haujawahi kuiacha timu pinzani salama na umekuwa ukitajwa na makocha pamoja na wachezaji wakubwa kuwa huwa wanapata tabu sana wanapokuwa uwanjani hapo sana sana kelele za mashabiki na muonekano wake.

Tokeo la picha la goodison park

Hebu tuiangalie kwa ufupi Everton hii mpya ambayo tangia kuanzishwa kwa ligi kuu ya England 1992 mpaka sasa haijachukua ndoo ya ligi kuu huku ikiambulia taji moja la kombe la FA .

Baada ya ligi kuu ya England kuanzishwa Klabu ya Everton ilianza kupoteza nguvu yake ya usajili ukilinganisha na vilabu kama Manchester United,Arsenal na Chelsea,Spurs,Liverpool na Manchester City ambazo zimekuwa zikisajili wachezaji wapya na wakubwa karibia kila msimu wakati hao Everton wakishindwa kusajili wachezaji wa karba hiyo kutokana na ukubwa wa gaharama.

Kwa miaka ya nyuma kuanzia 1990 kurudi chini mpira haukuwa biashara ulikuwa kiburudani zaidi ndiyo maana hata Everton waliweza kusajili wachezaji wakali kama mshambuliaji Dixie Dean ambaye aliweka rekodi kwa kutupia magoli 60 kwenye mechi 39 tuu za ligi ya soka ya Uingereza msimu wa 1927-28.

Picha inayohusiana
Dixie Dean

Je, nini kinaweza kuwarudisha Everton kwenye makali yao kama zamani? hapa ndiyo kuna uchawi kwani licha ya Vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu England kuingiza pesa nyingi kutokana na matangazo ya runinnga lakini bado kuna kusuasua kwa vilabu vidogo katika usajili ukilinganisha na vilabu vikubwa ambavyo vinapigana vikumbo kwa kugombania wachezaji wakubwa wenye viwango.

Kwasasa vilabu vingi ambavyo vinapigania ubingwa wa makombe makubwa kama ya Ligi na yale ya ngazi za vilabu barani ulaya, siri kubwa ipo kwenye usajili tena usajili mkubwa na kwa klabu kama Everton naiona kwenye picha hiyo kwani tayari kwa ujio wa Sportpesa kama wadhamini wakubwa wa Klabu hiyo wamemwaga mpunga wa maana ambao tumeona ukianza kufanya kazi kwenye usajili.

Everton ambayo tayari imetangaza rasmi kuanzia msimu ujao kuwa watakuwa chini ya udhamini na kampuni ya kubashiri ya Sportpesa dili ambalo ni kubwa katika historia ya klabu hiyo.

Tokeo la picha la Evertone sportpesa

Udhamini huo wa Sportpesa ambao unakadiriwa kuwa na dhamani ya Euro milioni 55 kwa mkataba wa miaka mitano utaifanya Everton kuingiza kiasi cha Euro Milioni 11.6 kwa kila msimu huku wakipewa ruhusa ya kuwa na wadhamini wengine kwenye viwanja vya mazoezi.

Hapo unaanza kupata picha wa wapi klabu hiyo inaelekea baada ya kusota kwa miaka 25 bila kuchukua taji la EPL.

wadhamini wao wa kwanza Chang ambao walidumu nao kwa miaka mitatu kuanzia 2014-2017 waliwalipa kiasi cha Euro milioni 16 tu pesa ambayo walikuwa wanalipwa Euro milioni 5.2 kwa kila msimu ndani ya miaka mitatu huku rais wa klabu hiyo, Robert Elstone akisema ndiyo dili ambayo ilivunja rekodi katika klabu hiyo kabla ya ujio wa udhamini wa Sportpesa.

Hapa unakuja kugundua kuwa hakuna shaka yoyote kuwa Everton ndani ya miaka mitano kuanzia msimu ujao itakuwa ni moja ya vilabu vya kuogopwa kwenye ushindani wa mbio za ubingwa wa ligi Kuu.

Katika vilabu vya ligi kuu England vinavyoongoza kuingiza pesa nyingi kupitia wadhamini  wao wa kwenye jezi ya kwanza ni Manchester United ambao wanalipwa kiasi cha Euro milioni 53 na Chevrolet, Chelsea wanalipwa Euro milioni 40 na Yokohama, Arsenal wanalipwa kiasi cha Euro milioni 30 na Emirates, Liverpool wanalipwa kiasi cha Euro milioni 25 na Standard Chartered, Manchester City wanalipwa kiasi cha Euro milioni 16 na Etihad Airways (UAE) huku nafasi ya sita ikienda kwa Tottenham Hotspurs ambao wanalipwa kiasi cha Euro milioni 16 na Kampuni ya AIA (China) .

Ukiangalia mtiririko huo unaona timu zote ambazo zinaingiza mkwanja mrefu ndiyo hizo hizo zinazofanya vizuri kila mwaka kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu England.

Hii inamaanisha kuwa kwa mpira wa kisasa jinsi ulivyo ni lazima uwe na pesa nyingi za kuwekeza ili kuweza kuwa mshindani kwenye kuwania makombe makubwa.

Klabu ya Everton sasa itakuwa klabu ya Saba kati ya timu 20 zinazoshiriki ligi kuu England kuingiza mkwanja mrefu kupitia udhamini wa matangazo kwenye jezi.

Hapa simaanishi ubingwa utakuja kirahisi ila namaaanisha kuwa Everton ndani ya miaka mitano ya udhamini wa Sportpesa watakuwa kwenye nafasi ya kushiriki michuano ya ngazi za vilabu barani ulaya kama UEFA na Europa League na kama watakaza basi halitakuwa jambo la kushangaza kuchukua ndoo ya ligi kuu England.

Unaweza ukabisha kwa kusema SportPesa wamefeli kwa Klabu ya Hully City utakuwa upo sahihi kwa upande mmoja kwani klabu hiyo ilikuwa inalipwa kiasi cha Euro milioni 3 tuu pesa ambayo kwa hali yoyote ile haiwezi kuifanya klabu hiyo kushindana na vilabu vikubwa.

Leicester City naweza kusema ndiyo klabu ambayo ilionesha maajabu kwa kuchukua ndoo msimu wa mwaka 2015/16 kwani haikutegemea sana usajili mkubwa bali ilitumia wachezaji wa kawaida na kuwakuza kuwafanya wakubwa wakati huo vilabu vikubwa vikiwa kwenye Transition ya kubadilisha makocha pamoja na wachezaji wakajikuta hao wakipata matokeo mpaka kuchukua ndoo lakini sio kitu cha kutegemea katika mpira wa kisasa na hili limeonekana msimu huu kwani mabingwa hao watetezi wamepata somo tosha.

Nakumbuka mapema mwaka huu baada ya Everton kutangaza dili hilo mtandao maarufu wa Daily Mail uliandika “Ujio wa Kampuni ya Sportpesa Everton ni changamoto kwa vilabu vya Spurs na Liverpool” hapa naona kabisa Everton watakuwa washindani wakubwa na pengine hata kurudisha heshima yao ya miaka ya nyuma.

Everton mpaka sasa wameshafanya usajili wa wachezaji wanne na tayari kuna tetesi imeanza kuwinda wachezaji wakubwa kutoka vilabu vya Barcelona na Celtic.

The Toffees watakuwa hapa nchini Tanzania tarehe 13 July mwaka huu kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya klabu ya Gor Mahia, mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu hii ni baada ya mshindi wa Sportpesa Super Cup kupatikana.

Sportpesa ambao ndiyo wadhamini wakubwa wa Everton na vilabu vya Simba, Yanga na Singida United kutoka Tanzania ambavyo tayari vimeonesha cheche za usajili wa mamilioni ili kujiimarisha kwa msimu mpya ujao.

Kwa nguvu hiii ya SportPesa hakuna shaka yoyote misimu miwili mbele tutarajie kuwaona Everton wakishiriki klabu bingwa barani ulaya au Europa kama sio kuchukua ndoo kabisa.

By Godfrey Mgallah

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents