Michezo

SportPesa kumwaga mamilioni kwa Watanzania kupitia promosheni ya Rafiki Bonus (+Video)

Kampuni ya Kubashiri ya SportPesa imezindua promosheni ya mtambulishe rafiki ijulikanayo kama RAFIKI BONUS ambapo wateja wa awali watajipatia bunus ya shilingi 2000/= kwa kila mteja mpya atakayemtambulisha kwa ajili ya kujiunga na SportPesa.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas.

Kwenye Promosheni hiyo ya RAFIKI BONUS mteja wa SportPesa ambaye tayari amekwisha jisajili, anachotakiwa kufanya ni kumshawishi rafiki/Ndugu ajiunge na SportPesa na akishajisajili na kuanza kucheza basi mteja wa zamani uliyemshawishi utapata Bonus ya Tsh 2000/= hii ni kwa mteja mmoja uliyemtambalisha.

“Kampuni yetu imekuja na Bonus Rafiki ikiwa kama njia ya kurudisha fadhila kwa wateja wetu na tunajua wamekuwa wakiwafundisha rafiki zao namba ya ya kubashiri na SportPesa, hivyo, basi tumeona ni vema na sisi tuwawekee mazingira ya wao kunufaika kwa uaminifu wao na kampuni, Bonus Rafiki inamuwezesha mteja wetu wa zamani kupata shilingi 2000 kwa kila mteja atakayemtabulisha katika jukwaa la kubashiri na SportPesa”,amesema Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas.

Ili mteja aweze kufuzu kushiriki promosheni ya RAFIKI BONUS anatakiwa awe amejisajili na awe mtumiaji wa SportPesa kwenye kubashiri, Pia mteja anayetambulishwa na rafiki yake anatakiwa atume neno KUBALI kisha kuandika namba ya simu ya mtu aliyemkaribisha katika jukwaa la kubashiri la SportPesa.

Vigezo vingine mteja mpya anatakiwa kuweka ubashiri angalau mara moja katika michezo ya Jackpot kwenye mchanganyiko wowote wa Multi Bet bila kujali aina ya mchezo , au kuweka Single Bet kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu yenye soko la njia tatu (1,x,2).

Mteja wa SportPesa anaweza kubashiri kwa njia ya ujumbe (SMS) au kwa njia ya tovuti kwa kubonyeza HAPA ili kushiriki bonus hiyo.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents