MichezoUncategorized

SportPesa waidhamini Yanga kwa Tsh Bilioni 5 (+Video)

Kampuni ya kubashiri ya SportPesa imetangaza rasmi kuingia mkataba wa udhamini na Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara msimu huu,Young Africans kwa miaka mitano.

Klabu hiyo itaingiza kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 5 huku wakianza kulipwa Shilingi milioni 950 kwa msimu ujao na ongezeko la asilimia 5% kila msimu.

Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Bw. Abbas Tarimba amesema fedha hizo zitagawia kwa awamu tatu ndani ya msimu mmoja lakini kutakuwa na bonus kwa kila kombe litakalochukuliwa na Yanga.

“Mbali na fedha zitakazotelewa na SportPesa pia kutakuwa na bonus ambapo kama Yanga watachukua ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao watapata bonus ya shilingi milioni 100 na bonus nyingine Kama wakifikia kila hatua kwenye michuano ya kimataifa kuna pesa watapata” alisema Abbas Tarimba.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga wakikabidhiana mkataba na CEO wa SportPesa, Pavel Slavkov.

Klabu ya Young Africans inakuwa klabu ya pili kudhaminiwa na Kampuni ya SportPesa nchini Tanzania baada ya mahasimu wao Simba kumwaga wino wiki iliyopita.

SportPesa kwa sasa ni mdhamini wa Klabu ya Hull City na Everton ambazo zinashiriki Ligi kuu England.

Pia nchini Kenya wanaidhamini Klabu ya Gor Mahia na AFC Leopards ambazo zinashiriki Ligi kuu ya nchi hiyo.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents