Michezo

Sportpesa waipa kiburi Everton: Yazipiku Chelsea na Arsenal kwa usajili wa kinda huyu

Klabu ya Everton ipo njiani kukamilisha usajili wa mshambuliaji chipukizi wa Nigeria, Henry Onyekuru kwa Euro milioni 7 kutoka klabu ya KAS Eupen ya Ubelgiji.

Tokeo la picha la Henry Onyekuru
Henry Onyekuru

Onyekuru (20), alifunga magoli 22 msimu uliopita katika klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ubelgiji msimu uliopita.

Mkurugenzi wa soka wa klabu ya Everton, Steve Walsh pamoja na meneja Ronald Koeman wameridhia kumchukua kinda huyo kama mbadala wa Romeru Lukaku ambaye yupo njia panda mpaka sasa kuihama klabu ya Everton.

Kinda huyo aliyekuwa anawindwa na klabu za Chelsea, Arsenal na West Ham United tayari ameshacheza mechi moja na timu yake taifa ya Nigeria katika mechi ya kirafiki dhidi ya Togo mapema mwezi huu ambayo walishinda 3-0.

Klabu ya Everton ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa itakuja nchini Tanzania mwezi ujao kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Gor Mahia.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents