Michezo

SportPesa wamwaga mamilioni ya udhamini Singida United (+Picha)

Baada ya kumalizana na Klabu ya Yanga SC na Simba SC, Kampuni ya Kubashiri ya SportPesa rasmi imetua Singida United kwa kusaini mkataba wa udhamini na Klabu hiyo kutoka mkoani Singida.

Katibu Mwenezi wa Klabu ya Singida United ‘Festo Sanga’ na CEO wa SportPesa, Pavel Slavkov.

Mkataba wa udhamini wa SportPesa na Klabu ya Singida United utakuwa ni wa mwaka mmoja na utakuwa na thamani ya Shilingi milioni 250 za kitanzania.

Kama tulivyokwisha wataarifu watanzania kuwa tumekuja SportPesa tumekuja kukuza Soka la Tanzania na sio Mpira wa miguu peke yake bali michezo yote na napenda niwajuze kuwa Kampuni yetu imeingia mkataba wa udhamini na Klabu ya Singida United, Mkataba ambao una thamani ya Shilingi Milioni 250 na ni wa Mwaka mmoja kuanzia mwaka 2017 hadi 2018“, Amesema Abass Tarimba Mkurugenzi mkuu wa SportPesa Tanzania.

Kwa upande wa Singida United hao wameahidi kutumia fursa hiyo ya udhamini wa SportPesa kusajili na kujitahidi kuchukua ubingwa msimu huu au kubaki nafasi ya pili ili kushiriki Michuano ya kimataifa.

Tumeipokea kwa Mikono miwili Kampuni ya SportPesa na wametufanya tuwe na uhakika wa kuchukua ubingwa msimu ujao au angalau nafasi ya Pili ili tushiriki michuano ya Kimataifa na hilo linawezekana sasa tutafanya kama Leicester City walivyofanya msimu uliopita na wanasingida wapo nyuma yetu kusindikiza timu yao“, alisema Katibu Mwenezi na Msemaji mkuu wa Singida United, Bw Festo Sanga wakati wa makabidhiano ya mkataba wao na SportPesa leo jijini Dar es salaam.

Kampuni ya SportPesa pia walitumia nafasi ya makabidhiano hayo ya Mkataba wa udhamini kwa kuonesha Jezi zitakazotumika na Singida United kwa msimu ujao.

CEO wa SportPesa, Bw. Pavel Slavkov akionesha Jezi mpya ya Singida United.

Hata hivyo Kampuni ya SportPesa imetangaza kuwa Udhamini wao kwa Singida United utakuwa wa Mwisho kwa Msimu huu ila wametangaza kuwa Msimu ujao mapinduzi yataendelea.

Tazama picha za hafla ya makabidhiano ya Mkataba huo wa udhamini kati ya SportPesa na Singida United.

Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba
Nahodha wa Timu ya Singida United, Nizar Khalfan akiwa na jezi mpya zitakazotumiwa na timu yake msimu ujao.

 

By Godfrey Mgallah/ Hamza Fumo

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents