Michezo

SportPesa wawatoa hofu mashabiki wa Simba, Yanga na Singida United

Kampuni ya kubashiri michezo nchini Tanzania ya SportPesa imewatoa hofu mashabiki wa mpira wa miguu hususani wa klabu za Simba, Yanga na Singida United kuwa yaliyotokea Kenya hayawezi kutokea Tanzania na kuahidi kuwa mwaka huu itaendelea kuongeza juhudi zake katika kuinua michezo nchini.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba

Taarifa hiyo imetoa taarifa hizo ikiwa ni siku mbili zimepita baada ya Kampuni ya hiyo nchini Kenya kufuta udhamini wake kwenye michezo yote nchini humo.

SportPesa wamesema dhama hiyo isijengeke kabisa kwa Watanzania kwani yaliyotokea Kenya yatabaki huko huko na kuwaahidi Watanzania kuwa mwaka huu imejipanga kuwekeza zaidi kwenye michezo mbalimbali.

Niziondoe hofu klabu za hapa nchini ambazo tumezidhamini za Simba, Yanga na Singida kuwa uamuzi tuliouchukua wa kusitisha udhamini kwa klabu za Kenya kuwa hauziusu klabu za hapa nchini. Hivyo, kama SportPesa tumepanga kuendelea kuzidhamini klabu hizo huku tukipanga kuendelea kuziboreshea zaidi udhamini kwa siku zijazo katika kuhakikisha tunaendeleza soka. Labda nimalizie kwa kusema kuwa, mwaka huu wa 2018 tumepanga uwe wa mafanikio zaidi katika kuhakikisha soka la nchini linapiga hatua hapa nchini,”amesema Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba leo alhamisi Januari 4, 2018 kwenye mkutano na Waandishi wa Habari.

Soma zaidi – SportPesa wasitisha udhamini kwenye michezo nchini Kenya

Kampuni ya SportPesa Tanzania inazidhamini klabu za Simba, Yanga na Klabu ya Singida United ambazo zote zinashiriki Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents