Michezo

SportPesa yaipa nguvu Singida United: Wanunua Basi la kifahari (Picha)

Baada ya kupata udhamini mnono kutoka katika kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa hatimaye klabu ya Singida United inazidi kutanua misuli yake katika ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kutambulisha usafiri wao utakao tumika katika kusafirishia wachezaji.

Basi la klabu ya Singida United (seheme ya nje)

Akizungumza na waandishi wa habari leo katibu Mwenezi wa klabu hiyo Festo Sanga amethibitisha Singida United kununua Basi jipya lenye gharama ya shilling milioni 350.

Katibu Mwenezi wa klabu ya Singida United, Festo Sanga

“Hili ni Basi aina ya Dragon ambalo limenunuliwa kwa fedha za klabu na linamilikiwa na Singida United hiyo ni moja ya jambo kubwa ambalo tunajivunia, kwa zipo timu ambazo mpaka sasa hazina usafiri lakini sisis kwa muda mfupi tunamiliki usafariki kama huu.

“Jambo la pili ni kuhusu maendeleo ya klabu , Singida United inatarajia kuanza kambi siku ya kesho mkoani Mwanza na wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi hata mmoja na tuna wachezaji 23 mpaka sasa. Kati ya wachezaji has wachezaji kumi na moja ni walewliopandisha timu na wachezaji sita ni wakimataifa.

“Uwanja wa Singida United unaendelea na ujenzi wake na tayari zimeshapandwa nyasi nyingine na zimeshaanza kuota kwa upande wa vyumba na majukwaa tayari na ujenzi umesimamiwa na Mkurugenzi wa Mkoa na Mkuu wa Mkoa na matarajio yetu michezo yetu ya nyumbani tutatumia uwanja wetu wa nyumbani” amesema kiongozi wa Singida United, Festo Sanga.

Kiongozi huyo amewataka wadau wa mchezo wa soka nchini kutambua klabu hiyo haifungamani na upande wowote kati ya timu kubwa nchini za Simba na Yanga kama inavyovumishwa.

 

Picha zinazofuata ni muonekano wa Basi hilo la klabu ya Singida United

Basi la klabu ya Singida United (sehemu ya mbele)

Basi la klabu ya Singida United (muonekano wa sehemu ya nyuma)

Basi la klabu ya Singida United (muonekano wa sehemu ya ndani)

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents