Michezo

SportPesa yaipunguzia mzigo serikali kuelekea Afcon U-17

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imesema ukarabati mkubwa wa ‘pitch’ ya Uwanja wa Taifa unaofanywa na Kampuni ya kubashiri ya SportPesa ni chachu kwa soka la Tanzania hasa hasa kuelekea katika maandalizi ya fainali ya kombe la Vijana la U-17  la Afrika mwaka 2019 zitazofanyika nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Ndugu Alex Mkeyenge

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Ndugu Alex Mkeyenge alieleza faida mbalimbali za ujio wa Everton nchini.

“Ujio wa Everton umekuwa neema kwetu sisi kama Wizara ya Michezo katokana na mipango mbalimbali waliyonayo kwenye suala zima la michezo. Marekebisho ya sehemu ya kuchezea (pitch) ya uwanja wa taifa yanayofanywa kuelekea mchezo wa Everton yataufanya uwanja wetu uweze kufikia viwango vya kimatifa na kutokana na kuwa na mechi hiyo itaonekana pande zote za dunia, tunaamini kuwa timu nyingine zitashawishika kuja kucheza Tanzania kutokana na ubora wa Uwanja,”  alisema Mkeyenge.

“Lakini pia matengenezo hayo yataisaidia Tanzania kuelekea maandalizi ya fainali za Kombe la Vijana la U-17 za Afrika mwaka 2019 zitakazofanyika nchini. Hivyo marekebisho haya yatakuwa yameipunguzia serikali mzigo mkubwa kuelekea maandalizi hayo ili iweze kuwekeza nguvu kwenye viwanja vingine hususani vya mikoani,” alisisitiza Alex.

Mapema alizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SportPesa Tanzania, Abbas Talimba alisema baada ya ukarabati mdogo walifanywa Uwanja wa Taifa kwaajili ya Everton, kutakuwa na ukarabati mkubwa zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents