Michezo

Sportpesa yakabidhi vifaa vya michezo na cheti cha shukrani kwa IGP Sirro

Kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa leo imechangia shilingi milioni ishirini na vifaa vya michezo ikiwemo jezi za nyumbani na ugenini na vilinda ugoko ‘shin guards’ kwa timu ya Jeshi la Polisi iliyopo daraja la kwanza.

Licha ya mchango huo Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kupunguza timu zake jambo ambalo wangekuwa na gharama kubwa za kuziudumia na hivyo kushindwa kufikia malengo.

Wakati huo huo, Abbas amelishukuru Jeshi hilo kwa msaada mkubwa waliyoutoa wakati wa ujio wa klabu ya Everton hapa nchini hali iliyosababisha kupata heshima kubwa duniani kiasi kwamba ziara hiyo kushirikishwa katika filamu inayojulikana kama  “Best Brand Activation Involving Football”  na hivyo kulikabidhi Jeshi hilo cheti kinachotambua mchango na ushiriki wake katika ujio wa kikosi hicho cha Uingereza.

Tarimba Abbas amesema kuwa “Katika kukukabizi vitu hivi lakini pia tutakupa Certificate of Appreciation, hii kitu imetokana na msaada mkubwa sana najua ni wajibu wenu lakini mmejitoa kutusaidia wakati wa kuwasili kwa Everton”, amesema Tarimba Abbas.

Mkurugenzi huyo wa Sportpesa Abbas ameongeza “Tumepata heshima kubwa sana duniani pengine watu hawa jui lakini tumepata heshima kubwa sana kiasi kwamba ujio wa Everton kumetengenezwa filamu ambayo inashiriki na imekuwa ‘nominated’ kushiriki katika kitu wanaita ‘Best Brand Activation Involving Football’ katika dunia. Tanzania hii ya Everton in Tanzania tunashindana na nchi nyingine mbili na hii ya kwetu ni ya tatu hii yote isingeweza kufanikiwa ila ni ushiriki wa wadau wengi wametusaidia”.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro ameishukuru kampuni hiyo ya Sportpesa kwa kuchangia fedha na vifaa vya michezo kwa timu ya Jeshi hilo nakuahidi fedha hizo kutumika kama zilivyokusudiwa.

“Nikupongeze sana Mkurugenzi, Abbas kwa hili mlilolifanya Sportpesa imetoa sapoti kubwa nyinyi ni wadau wetu” amesema Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro.

“Kuna wadau wa aina mbili kuna wadau welevu wanasema smart partners na kunamdau ambaye yupo tu ambaye unashindwa kujua muelekeo wake lakini kimsingi Sportpesa ni mdau mwerevu ameona umuhimu wa kuchangia fedha pamoja na nguo za michezo kwaajili ya kusapoto Jeshi la polisi hii itatusaidia sana kwa sababu tukicheza michezo tutakuwa karibu sana na jamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents