Michezo

SportPesa yatua kwa kishindo, yatoa milioni 50 kwa Serengeti Boys

Kampuni ya Mchezo wa kubashiri wa SportPesa imezinduliwa rasmi hii leo nchini,ikiahidi kuhakikisha inasaidia kuinua michezo hapa nchini Tanzania. Katika kuhakikisha hilo Kampuni hiyo imetoa mchango wake wa Sh Milioni 50 kwa ajili ya timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17, ”Serengeti Boys”, ikiwa na lengo la kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa katika michuano yake nchini Gabon ambayo ni ushiriki wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Dunia.

Viongozi wa SportPesa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa    Habari,tamaduni,sanaa na micezo,Dk Harrison Mwakyembe.

Mkurugenzi wa SportPesa hapa nchini, Abbas Tarimba, ameahidi kutoa mchango huo katika kuunga juhudi za watanzania pamoja na waziri wa habari,utamaduni, sanaa na michezo, Dk.Harrison Mwakyembe kama alivyo elezea.

“SportPesa Tanzania, tumefikiria ni kwa namna gani tunaweza kuichangia Serengeti Boys, na kwa haraka tu utawala umethibitisha kuchangia kiasi cha shilingi Milioni 50, kwahiyo nimtoe machungu Waziri, kuja kwake peke yake kumeitengenezea Serengeti Boys Milioni 50” alisema Tarimba”.


Mkurugenzi wa SportPesa hapa nchini,Abbas Tarimba

Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ni waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, ameishukuru kampuni hiyo kuja hapa nchini na kuwekeza zaidi kadri iwezavyo ikiwa na lengo la kutoa mchango mkubwa katika michezo.


Waziri wa habari,tamaduni,sanaa na michezo Dk Harrison Mwakyembe,   akiikaribisha kampuni ya SportPesa, katika uzinduzi wake leo.

“KARIBU sana, na wacha nitumie na fursa hii kukuhakikishia serikali ipo pamoja na wewe na kwa kifupi niseme karibu. Hii ni nchi ya michezo, ndugu zangu watanzania mimi nimeiona hii ni fursa pekee ya kuendeleza michezo nchini na fursa hii hatuiachii”

“SportPesa, inaendesha michezo ya kubahatisha, tumeskia wote hapa kwamba hii kapmuni inawekeza katika michezo, na tumeona walichofanya kwenye nchi nyingine, watanzania hii ni nafasi pekee katika michezo hapa nyumbani, na tunasema karibuni na tutawaunga mkono katika jitihada zenu”.

“Wazungumzaji waliokuja hapa wameemsa tunataka tuwatengeze wakina Mbwana Samatta, na ninataka kuwahakikishia viongozi wa SportPesa, kwamba Tanzania kuna wakina Mbwana Samatta wengi sana, wengine wapo tayari wala hauhitaji kuwatengeneza ni kuwapromote tu. Ninao sasa hivi wakina Mbwana Samatta 22 wanaitwa “Serengeti Boys” ni kuwanyanyua tu waende kuonyesha maajabu duniani” alisema Mwakyembe

Mapema asubuhi ya leo, kampuni hiyo imefanya uzinduzi wake rasmi huku Tarimba akielezea mafanikio makubwa yaliopatikana nchini Kenya kupitia kampuni hiyo ambayo kwa sasa inadhamini ligi ya Kenya pamoja na kuiwezesha michezo mingine zikiwemo michezo ya ngumi, Rugby nk.


Uzimduzi rasmi wa Kampuni ya SportPesa Tanzania.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe, amesema kuwepo na usimamizi makini hapa nchini ni miongoni mwa chachu ya SportPesa kuwavutia kuja kuwekeza hapa nchini.

“Katika muda mfupi, michezo ya kubashiri matokeo hapa nchini imekuwa na mafanikio makubwa sana, kwa miaka miwili iliyopita yani mwaka 2015/16 kupitia michezo ya kubashiri matokeo tuliweza kukusanya Bilioni 21.8 na tukapeleka serikalini”.

“Kabla ya hapo hela nyingi ilikuwa inatoka katika tasnia ya kasino ambayo sasa hivi tunao ingawa inapitwa na wakati maana miaka miwili, Sport Betting imefikisha 21.8 wakati kasino imefikisha 21.2 kwa hiyo tunaamini kabisa kwamba Sport Betting itakuwa sana katika miaka ijayo na hasa kuzingatia kwamba SportPesa sasa wameingia katika soko” alisema Mbelwa.


Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe.

Sport Pesa pia ni mshiriki rasmi wa michezo ya kubashiri kwa klabu kubwa katika Ligi Kuu za England zikiwemo – Arsenal na Southampton ambao kupitia ushiriki huu, wameweza kutoa mchango wa mafunzo mbalimbali kwa timu kubwa za mpira wa miguu nchini Kenya,.

Hapa nchini tayari kuna fununu kuwa kampuni hii ya SportiPesa ipo katika michakato ya ya mwisho ya kuingia mikataba ya kuzidhamini klabu kongwe za soka hapa nchini, Simba SC pamoja na Yanga, ingawa katika hilo halijawa na uhakika wa kuzungumziwa.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents