Michezo

SportPesa yawakutanisha Everton FC na Mbwana Samatta

Klabu ya Everton ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya kubashiri ya SportPesa inatarajiwa kuvaana na klabu KRC Genk ya Ubelgiji ambayo anakipiga Nahodha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta.

Tokeo la picha la everton fc sportpesa
Everton

Kupitia ukurasa wa Twitter wa klabu hiyo wamethibitisha taarifa hizo kuwa watacheza na timu hiyo mwezi ujao mnamo tarehe 22 July.

Everton ambayo itakuwa nchini Tanzania mwezi ujao Tarehe 13 July kuvaana na Klabu ya Gor Mahia ya Kenya kwenye mchezo wa kirafiki ulioandaliwa na Wadhamini wao SportPesa viongozi  wake wamesema mechi zote za Pre Season kwao zitakuwa ni Mechi muhimu kwani ni muda wa kujipima kabla ya msimu mpya kuanza.

Maandalizi ya mchezo wa Everton dhidi ya Gor Mahia yameanza kupamba moto nchini kwa matengenezo ya uwanja wa Taifa utakaotumika kucheza mechi hiyo huku wadau wa soka wakiwa na shauku ya kuwaona Everton.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents