Michezo

SportPesa yawapa kiburi Singida United: Yasajili watano kutoka AFCON (Video)

Badaa ya kuhakikisha wamemalizana na klabu kongwe Yanga na Simba SC kwa kuingia nao mikataba minono itakayowezesha klabu hizo kufanya maandalizi mazuri kwaajili ya msimu ujao, Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa imeingia mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Singida United wa mwaka mmoja na SportPesa ambao thamani yake ni Milioni Tsh. 250

Katibu Mwenezi wa Klabu ya Singida United ‘Festo Sanga’ na CEO wa SportPesa, Pavel Slavkov.

 

Katibu Mwenezi wa Klabu ya Singida United ‘Festo Sanga’
“Nadhani SportPesa wameona Singida United ina mikakati,ina mikakati kwa maana tumeshaonyesha uwezo binafsi kama klabu kusajili Kocha kama , Hans  Van  Pluijm, ambaye ni kocha Mkubwa ambae klabu kama Simba SC na Azam FC zilikuwa zikimng’ang’ania lakini klabu ambayo imepanda Daraja na kumchuku hiyo ni moja yakitendo ambacho inaonyesha hii klabu ipo Siriasi”.

Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba

“Singida United wanaweza wakawa ni chachu ya timu nyingine , za maeneo ya pale vilevile nayo yakakuwa kama ambavyo singida wameweza kukua hivyo ndio sababu kubwa iliyotufanyisha sisi kuingia Mkataba na Singida United”

 

Nizar Khalfan Mchezaji wa klabu ya Singida United.
“Naweza kusema unaweza kuleta mabadiliko makubwa ukiangalia timu tatu ambazo tumepata mkataba huu, na kwetu sisi pia imetupa nguvu kiasi kikubwa ya kujituma sababu ukiangalia wametupa mkataba wa mwaka mmoja na timu nyingine zimechukua mkataba zaidi ya kwetu sisi kwahiyo sisi tutafanya kazi kubwa ili mkataba huu ukiisha waweze kutuongeza mingine”.


BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents