Aisee DSTV!
SwahiliFix

Spotify wakiri kufanya makosa kufuta nyimbo za R.Kelly na XXXTentacion

Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Spotify, Daniel Ek, amesema kuwa walifanya makosa kuzifuta nyimbo za R.Kelly na XXXTentacion kwenye Playlist zao.

Bosi huyo wa Spotify amesema hayo Jumatano hii wakati alipokuwa kwenye mahojiano na Recode. Daniel Ek amezungumza kuhusiana na sera zao mpya za kufuta ngoma za wasanii kwenye playlist kutokana na contents zenye lengo la chuki na miendeno mibaya ya wasanii

“Tulifanya makosa, tungeweza kufanya kazi nzuri zaidi. Lengo lote hilo lilikuwa ni kuhakikisha kwamba hatukuwa na chuki kwenye huduma. Haijawahi kuadhibu mtu mmoja,” amesema Daniel Ek.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa lengo la sera mpya lilikuwa ni kuhakikisha hawa promote maneno na lugha ya chuki kwenye mtandao wao na lengo halikuwa kumuadhibu msanii fulani kama inavyoonekana sasa hivi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW