Michezo

Spurs yafanya mazoezi Santiago Bernabeu (Video + Picha)

Kikosi cha Tottenham Hospur tayari kimeshatua nchini Hispania na hapo jana siku ya Jumatatu kimefanya mazoezi mepesi katika dimba la Santiago Bernabeu kujiweka sawa dhidi ya mwenyeji wake klabu ya Real Madrid kwenye mchezo wao wa klabu bingwa barani Ulaya ‘UEFA’ utakao pigwa leo.

 

Kikubwa kinachozungumzwa kwa wadau wa mchezo wasoka ni kukutana kwa Cristiano Ronaldo na mchezaji wa Spurs, Harry Kane ambao wanakaribiana kwa uwiano wa kufunga magoli katika kundi lao.

Kane amefunga jumla ya mabao matano katika michuano hiyo ya klabu bingwa barani Ulaya waka Ronaldo ametupia magoli manne katika kundi H.

Hatuendi Bernabeu kumshanga Ronaldo – Pochettino

Kitu kingine kinachofanya mchezo huo kuwa gumzo kwa wapenzi wa soka ni kufuatia mabingwa hao wa tetezi wa klabu bingwa barani Ulaya, Madrid kuhitaji kumsaini mchezaji wa Spurs, Harry Kane.

Picha za kikosi cha Tottenham Hospur 

)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents