Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Staa wa Burundi afunguka kuhusu Bongo Flava na wasanii wanaokubalika zaidi kwao

By  | 

Msanii wa Burundi, Gaga Blue ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Ivo Ivo’ aliomshirikisha rapper Young Dee, amefunguka kuhusu muziki wa Bongo Flava nchini humo pamoja na wasanii wanaokubalika zaidi.

Akiongea na Bongo5, muimbaji huyo ambaye pia amefanya ngoma na Young Dee, amesema muziki wa Tanzania upo juu zaidi Burundi kwa kuwa wanajua kufanya mipangilio mizui ya nyimbo zao na kubrand muziki wao uweze kufika mbali zaidi.

“Muziki wa Tanzania na Burundi hauna tofauti sana, ila Tanzania wanajua kuplan na wanajua kuband muziki pamoja na kufikisha muziki mbali ndio maana nimekuja hapa na mimi kwa sababu wote tupo East Afrika ni kitu kimoja. Lakini kwa kuimba na kila kitu hakuna tofauti ya Tnazania na Burundi,” amesema.

Msanii huyo ameendelea kwa kufunguka kwa msanii wa Bongo Flava ambaye ngoma zake zinapigwa sana nchini humo amesema, “Unajua Burundi hakuna ubaguzi msanii yoyote anayefanya vizuri nyimbo inakuwa hewani inapigwa kila Tv na kila radio. Ninaweza kusema wasanii wote wanaofanya vizuri kazi zao zinakuwa zinapokelewa vizuri na zinachezwa bila ubaguzi.”

Gaga ameendelea kwa kusema Alikiba na Diamond wote ni wasanii wanaofanya vizuri nchini Burundi huku ngoma zao zikipigwa mara kwa mara na hata walivyowahi kufanya show nchini humo kila mmoja alifanikiwa kupata nyomi ya kutosha.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW