Habari

Staa wa filamu ya Hotel Rwanda ashitakiwa kwa ugaidi

Kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mmoja wa wapinzani wakuu wa serikali ya Rwanda Paul Rusesabagina amefikishwa kizimbani mjini Kigali nchini Rwanda akikabiliwa na mashitaka ya ugaidi.

Paul Rusesabagina alipata umaarufu mkubwa kupitia filamu maarufu kama Hotel Rwanda ya mwaka 2004.

Anashutumiwa kuendesha mauaji ya raia wasio na hatia kupitia mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa FLN kusini magharibi mwa Rwanda miaka miwili iliyopita.

Paul Rusesabagina amefikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo ya wilaya ya Kicukiro mjini Kigali kujitetea dhidi ya kusikilizwa kesi yake akiwa nje au akiwa rumande.

Lakini baada ya kufikishwa kizimbani kutwa nzima ilikuwa kuhusu ikiwa mahakama hiyo ina mamlaka kwa mujibu wa sheria kusikiliza kesi yake au la.

Mawakili wake walionyesha vipingamizi vya aina tatu huku wakishikilia kwamba mahakama hii haina mamlaka ya kuendesha kesi yake.

Mawakili wake pia wamesema kwamba kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika wilaya jirani ya Gasabo kwa sababu ndipo mtuhumiwa ana makazi.

Jambo jingine mawakili wamesema kwamba mashtaka yanayomkabili aliyatenda akiwa nchini Ubelgiji na kwamba kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni mikutano ya hadhara ambayo aliifanya na kwamba alikuwa na uhuru na haki ya kuifanya mikutano hiyo.

Kuhusu uraia wa mshukiwa upande wa mashtaka umesema kwamba, Paul Rusesabagina hakuwahi kupoteza uraia wa Rwanda kwa mujibu wa sheria na kwamba kisheria anachukuliwa kama raia wa Rwanda licha ya kuwa na uraia wa nchi nyingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents