Burudani

Staa wa Isidingo, Rajesh Kumar akwea Mlima Kilimanjaro

Muigizaji wa tamthilia ya Isidingo: The Need, Jack Devnarain maarufu kwa uhusika wake kama Rajesh Kumar amekwea mlima Kilimanjaro.

1000434_827825

Devnarain na watu wengine zaidi ya 30 kutoka nchini Afrika Kusini walipanda mlima huo wiki hii. Alialikwa na taasisi ya Nelson Mandela Centre of Memory kama sehemu ya kampeni ya Trek4Mandela.

Kampeni hiyo inatumika kukusanya fedha kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kike 270, 000 wanaoshidwa kwenda shule kutokana na kukosa vitu mbalimbali kwaajili ya usafi zikiwemo pedi za kutumia wakati wa hedhi.

Devnarain anatarajia kukusanya randi milioni moja kwaajili ya kampeni ya Caring4Girls.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents