Burudani

Video: Staa wa muziki Zanzibar adai utandawazi umefelisha muziki wao

Msanii wa muziki kutoka Zanzibar, Mustapha Yusuph maarufu kama Smile amebainisha kinachowafelisha wasanii wa kisiwani humo kutofanya vizuri nje ya mipaka ya kisiwa hiko.

Akiongea na Bongo5, Smile amesema kuwa licha ya muziki unadaiwa kuanzia kisiwani humo ila kumekuwa na changamoto ya wasanii kutojulikana sana kama ilivyo kwa wasanii wengine kutoka huku Bara.

“Ingawa muziki ulianza Zanzibara, watu wanasema lakini sisi huku kidogo utandawazi ulichelewa na watu kutojua kuwa sanaa inatakiwa ipewe kipaumbele kwa Zanzibar. Nafikiri kwa sasa hivi kidogo watu wanaanza ile sanaa kuipa kipaumbele na kuona umuhimu wake katika jamii,” amesema msanii huyo.

“Tunataka tuondoe dhana katika jamii kuwa muziki ni uhuni, wetu huku imechelewa kuondoka ile. Ingawa Dar wamewahi kuiondoa lakini mpaka sasa kwetu bado wanayo ile muziki ni uhuni,” ameongeza.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents