Habari

Staa wa NBA, Dirk Nowitziki aoa mkenya

Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu kwenye Ligi ya NBA ya Marekani wa timu ya Dallas Mavericks, Dirk Nowitzki amefunga ndoa ya kitamaduni nchini Kenya na mke wake Jessica Olsson.
Sherere hiyo ilifanyika katika utamaduni wa kabila la kikuyu uitwao Ngurario.
Harusi hiyo ya kimya kimya, ilifanyika weekend ya July15 lakini habari zimejulikana jana. Mama yake Jessica ni mkenya huku baba yake akiwa mtu wa Sweden.
Kaka zake wawili Martin na Marcus Olsson wanacheza soka la kulipwa kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Dirk Werner Nowitzki ni mzaliwa wa Ujerumani ambapo mwaka jana aliiongoza timu yake ya Mavericks kwenye fainali za NBA na kuchukua ubingwa kwa kuishinda timu ya Miami Heats.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents