Burudani

Staa wa ‘Straight Outta Compton’ akamatwa kwa tuhuma za ugaidi

Staa wa filamu ya ‘Straight Outta Compton’, R. Marcos Taylor aliyeigiza kama Suge Knight amejikuta mikononi mwa polisi kwa kutuhumiwa kufanya kitendo kinachohusishwa na ugaidi.

R. Marcos Taylor aliyeigiza kama Suge Knight

Taylor anadaiwa kuwa alimtishia moja ya muhudumu wa TD Bank iliyopo New Jersey, Marekani kumuua baada ya kadi yake ya bank kusumbua. Tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 8 mwezi nane mwaka huu.

Shuhuda wa tukio hilo amelielea jeshi la polisi kuwa Taylor, alimtishia mfanyakazi wa benki hiyo kwa kumtakia kuwa atamuua.

Baada ya polisi kufika katika eneo hilo walikuta mzozo na kumkamata muigizaji huyo na pia amefunguliwa mastaka yanayohusiana na kigaidi. Hata hivyo Taylor alijitetea kwa polisi hao na kusema kuwa muhudumu huyo anauadui.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents