DStv Inogilee!

Stamina adai ROSTAM kwa kipindi hiki watayumba kidogo, aeleza sababu kwa uchungu (+video)

Moja ya rappers wanaounda kundi la ROSTAM, Stamina amesema kuwa kundi hilo kwa sasa litapitia changamoto kwa kipindi kifupi, hii ni baada ya kifo cha Ruge ambaye alikuwa anawapa ushauri na sapoti kubwa kwenye kundi hilo.

Stamina akiongea na Bongo5, amesema kuwa Ruge alikuwa ni mtu mwenye umuhimu sana kwenye kundi la ROSTAM na alikuwa anawasaidia hadi namna ya kupanda jukwaani.

Akiongelea kuhusu pengo hilo, amesema kifo cha Ruge sio kimewaumiza hao tu, bali ni pigo kwa wasanii wengi kwani Ruge alikuwa na mchango mkubwa kwa vijana wengi.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW