Burudani

Stamina aitetea ‘Like Father like Son’ kuwa haijabuma, adai inafanya vizuri mikoani kuliko Dar

Rapper Stamina amesema kuwa wanaosema kuwa collabo yake na Fid Q ‘Like Father Like Son’ imebuma, labda wanasikiliza radio za Dar peke yake kwasababu ana uthibitisho wa ngoma hiyo kufanya vizuri kwenye radio za mikoani.

Stamina

Hata hivyo amekiri kuwa ni kweli ‘Like Father Like Son’ haijafanya vizuri kama ngoma yake na Nay ‘Huko Kwenu Vipi’, lakini amesisitiza kuwa hiyo ni kutokana na utofauti wa nyimbo hizo mbili.

“Ngoma zina utofauti ilipofika hii mimi ninashukuru kabisa ukisema kwamba imedrop nakubishia kwasababu, labda kama unasikiliza tu radio za Dar es salaam, kwasababu nasikiliza sana radio za mikoani, Interviews nyingi […] ukisema imedrop yaani hapo majibu yake sina kwasababu nina evidence nyingi za radio za mikoani, labda haija hit kama ‘Huko kwenu vipi’. Tofauti ya ngoma we sikiliza ‘Like Father Like Son’ na ‘Huko Kwenu vipi’ ni miziki miwili tofauti, miziki ya kubishanabishana mara nyingi inakuwaga inafika, Watanzania wanapenda vitu kama vile.” Stamina aliiambia Genge ya E-FM inayoongozwa na Ezden na Baghdad.

Aliongeza,
“Tumedrop hiyo (Like Father Like Son) kwaajili ya kuondoa ukimya pia, leo nimetoa ngoma hii, kesho nimetoa ngoma ya mapenzi, kesho kutwa nimeimba sijui siasa, muziki ndio unavyoenda sio tunaimba kitu kimoja kila siku hivyo hivyo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents