Burudani

Stamina amchukua Vanessa Mdee kuipa nguvu ngoma yake mpya

Rapper Stamina ameamua kumchukua Vanessa Mdee kuupa nguvu wimbo wake mpya utakaotoka mwezi huu.

Stamina

Stamina amedai kuwa atahakikisha wimbo huo unatoka pamoja na video ili kuepuka makosa yaliyojitokeza kwenye wimbo uliopita ‘Uko Kwenu Vipi?’ aliomshirikisha Nay wa Mitego.

“Wiki kama sio moja au mbili zijazo nitatoa wimbo mpya niliofanya na Vanessa Mdee ambayo tayari umeshafanyika ila this time sitaki kukosekana kwenye video kama mwanzo,” rapper huyo ameiambia Bongo5.

“Nataka kuanza na video kabisa. Kwa sasa hivi ndo tunapanga issue za kushoot nataka wakati ninarelease wimbo tayari nina video mkononi. Sitaki tena kufanya makosa nataka niwahishe video. Ngoma imefanyika Kili Records na producer wawili.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents