Burudani

Stamina na Roma ‘ROSTAM’ wapiga show na mavazi ya viwandani jukwaani, wenyewe waeleza sababu ya kufanya hivyo (video+picha)

Rapper Roma Mkatoliki na Stamina (ROSTAM) jana waliitikisa Mbagala kwa kufanya bonge la show kwenye Ninogeshe Music Concert ambapo kitu cha kushangaza walipanda jukwaani wakiwa wamevalia mavazi ya viwandani.

Roma Mkatoliki aliyevaa Ovaroli jekundu akiwa na Stamina jukwaani.

Wakizungumza baada ya show hiyo, wawili hao wamedai kuwa wamevaa sare hizo za viwandani ili kuunga mkono sera ya Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.

Wakati Mwingine Tunahisi kama Kiwanda Chetu Cha Burudani (Muziki Bongo Flavour) Hakitolewi Macho Na Kupewa Thamani Na Kipaumbele Kama Inavyostahili Kwa Mapana Na Ukubwa Wake. Sisi Kama #ROSTAM (Roma Na Stamina) Tunajaribu Kuonyesha Kuwa Hiki Ni Kiwanda Na Kinazalisha Na Kutoa Ajira Kwa Vijana Wengi Sana. Na Hii Ndiyo Sababu Iliyotupelekea Kuvaa Mavazi Haya Ya Kiwandani Tukiwa Jukwaani Tunaimba Parapanda. Bongo Flavour ni kiwanda kitoleeni macho tuiishi kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda.“wamesema ROSTAM.

Tazama picha na video za wawili hao walivyoitifua Mbagala.

https://youtu.be/YEB9Bpdxo7U

Related Articles

12 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents