Burudani

Stamina, Roma ‘wazikacha’ team Zari na Wema

Baada ya kuachia ngoma yao ya pamoja ‘Wapinzani wa Jadi’ ambayo inawakilisha umoja wao ‘ROSTAM’, Roma amesema walivyoimba katika ngoma hiyo vinawakilisha makundi fulani katika jamii na siyo wao kujivika hilo katika maisha yao.

B Dozen, Stamina, Roma na Mamy Baby

“Idea ni wapinzani wa jadi na tulijaribu kutengeneza zile stori ambazo mnaweza kukaa katika sehemu, vilinge mkapiga stori, haiwakilishi Roma na Stamina ila inawakilisha masikani nyingi vinaweza vikaweza vikatokea,” Roma ameiambia XXL ya Clouds Fm na kuongeza.

“Kuna mtu siyo team Wema wala team Zari lakini ilimradi mwenzake kamtaja Wema yeye anataka kuwa against, kwa hiyo haimaanishi real life kwamba Roma ndio moja kwa moja katika baadhi ya vitu lakini hoja ambayo tulikuwa tunataka tuiwakilishe inafika wakati wale wapinzani wa jadi wanakuwa kama wanaenda sawa,” amesema Roma.

Kwa hatua nyingine Stamina amesema, “hii ndio project ya kwanza ya ROSTAM na kitu kizuri tumemaliza kurekodi albamu, sisi sio kundi sisi ni familia mbali na muziki tuna maisha yetu ya binafisi , tunasaidiana, tunaambiza ukweli, kwa hiyo tumeona ukaribu wetu tunaweza kuuweka kwenye muziki”.

Kwa sasa Roma anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Zimbabwe’ wakati Stamina akitamba na International Local.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents