Burudani

Stamina: Sijawahi kuona mtu aliyesoma vitabu vingi kama Fid Q

Rapper kutokaka Morogoro Stamina amesema ni msomaji mzuri wa vitabu lakini hawajahi kukutana na mtu aliyesema vitabu vingi kama alivyosoma Fid Q.

“Sisi huwa tunasoma vitabu ambavyo vina upeo mkubwa lakini siwezi kumfikia yule jamaa (Fid) yule jamaa kasoma bana, kasoma vitabu vingi sana kwasababu kama Ben Carson ni series unajua ile… ya vitabu, jamaa yuko mbali sana, yuko kitabu cha 48 sijui huko rafiki yangu mimi ndo kwanza naenda na ishirini ishirini ngapi huko yaani jamaa yuko deep sana kwenye usomaji wa vitabu,” amesema Stamina kwenye interview na Bongo5.

Stamina amesema usomaji wa vitabu umempa upeo mkubwa wa kufikiri na kukitolea mfano kitabu cha Ben Carson, Think Big.

Amesema Fid Q anamchukulia kama baba yake kimuziki ambaye amekuwa akimwelekeza mambo mbalimbali katika uandishi na amekiri kuwa amemsaidia kwa kiasi kikubwa.

Katika kudumisha uhusiano wa baba na mwana kwenye muziki, Stamina amemshirikisha Fid kwenye ngoma yake itakayotoka November 14 mwaka huu iitwayo Ushauri Nasaha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents