Michezo

Stanley Okumbi ateuliwa kuwa kocha mpya wa Harambee Stars

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars imepata kocha mpya ambaye ni Stanley Okumbi anayechukua nafasi ya Mscotland, Bobby Williamson aliyeondoka.

mathare-united-coach-stanley-okumbi-was-a-happier-man-after-winning-against-nakuru-all-stars_1bsttb1me01pz1ijbsk5cohqhk

Kocha huyo wa zamani wa timu za vijana za Kenya ataiongoza Harambee Stars katika mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.

Nick Mwendwa ambaye ni mwenyekiti mpya wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), amesema mwishoini mwa wiki kwamba, Okumbi, aliyeifundisha timu ya Ligi Kuu ya nchi hiyo, Mathare United msimu uliopita, atakuwa kocha wa muda wa Harambee Stars itakapomenyana na Guinea Bissau ugenini mjini Bissau mwezi ujao.

Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Kenya, Musa Otieno, aliyekuwa Msaidizi wa Williamson ataendelea kuwa Kocha Msaidizi Harambee Stars chini ya Okumbi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents