DStv Inogilee!

Star wa muziki Davido wa Nigeria atiwa mbaroni kwa tuhuma za kutumia fedha bandia katika club ya usiku nchini Hungary!

Weekend iliyopita superstar wa Nigeria na msanii mwenye mafanikio David Adeleke a.k.a Davido amejikuta akitiwa mbaroni huko Budapest, mji mkuu wa Hungary kwa tuhuma za kutumia fedha bandia katika night club ya Budapest usiku wa June 22.

Davido

Mtandao wa Naija Gist wa Nigeria umeripoti kuwa, inasemekana akiwa na kaka yake mkubwa na meneja wake walikamatwa na kupelekwa polisi wakituhumiwa kutumia fedha bandia za euro katika club moja ya usiku.

Davido anayetegemewa kutumbuiza jukwaa moja na star wa Tanzania Diamond Platnumz mwezi ujao (July 27) nchini Kenya, alikamatwa baada ya kutoa pesa hizo kwaajili ya kulipia vinywaji ndipo iligundulika ni hela bandia.

Kabla ya kuwasili Hungary, Davido na watu wake walitokea nchini Italy ambako aliperform katika concert (June 21).

Kaka yake na Davido aitwaye Adewale Adeleke baada ya kukamatwa alidai kuwa pesa hizo (fake currency) walipewa kama malipo na promota wa Italy walikotokea kabla ya kutua Hungary.

Masaa machache baada ya kufikishwa polisi Davido na wenzake walitolewa majira ya saa 8 usiku (June 23)baada ya promota wa Budapest kuwasili na kuwaokoa.

Msanii huyo na crew yake kwa sasa wako jijini Paris, Ufaransa tayari kwa show nyingine inayotegemewa kufanyika Ijumaa hii (June 28).

Kwa mujibu wa mtu wa karibu inadaiwa kuwa star huyo wa Nigeria aliwaomba baadhi ya vyanzo vya habari vya karibu kuficha habari ya kukamatwa kwake ili isimharibie show zake zinazokuja, too bad kwa Davido sababu habari tayari iko mtandaoni!

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW