Michezo

Stars Kuwaua Waarabu Oktoba 9

Kocha wa timu ya Taifa Tanzania,Taifa stars Jan Borge Poulsen jana ametangaza kikosi cha majina 23 kitakacho ivaa Morocco kuwania kufuzu katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika 2012 na kusema atatumia mfumo wa 4-2-3-1 kuwaua waarabu hao watakapo kutana kwenye uwanja wa Taifa Oktoba 9.

Kwa kutumia mfumo huo ,Poulsen alisema watacheza kwa kushambulia na kuzuia pale itakapo hitajika kufanya hivyo.

Mfuumo huo ambao umekuwa ukitumika na klabu za Hispania na Ufaransa,ndio iliyo iwezesha Ufaransa kuichapa Brazil 3-0 na kutwaa kombe la Dunia mwaka 1998. Waliutumia tena mfuo huo kwenye kombe la Dunia 2006 na ikawasaidia tena kuwafunga Brazil bao 1-0 katika robo fainali iliyopelekea kuwatupa nje ya michuano hiyo.

Pia mfumo huo ulitumiwa wa Fabio Kapello na kuisaidia Real Madrid kushinda taji la La liga huku akiwatumia viungo Beckham na Robinho kama mawinga na Emerson na Diara kama viungo wakabaji.

Rafa Benitez aliwahi kutumia mfumo huo wakati akiifundisha Valencia na kuisaidia kushinda makombe mawili ya La liga na UEFA Cup.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents