Michezo

Stars yatakata COSAFA, Mzamiru akipaisha Kiswahili (Video)

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imezidi kutakata katika michuano ya COSAFA inatuendelea kutimua vumbi nchini Afrika Kusini, baada ya hapo jana kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Angola ikiwa ni mchezo wa kundi A, uliopigwa katika uwanja wa Royal Bafokenge.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakiingia uwanjani

 

Stars ambayo inaongoza kundi hilo ikiwa na alama nne ikiwa tofauti ya goli moja na timu inayoshika nafasi ya pili, sasa inajipanga katika mchezo wake wa mwisho ambao watacheza Alhamisi hii dhidi ya Mauritius huku wapinzani wao wakaribu Angola wakivaana na Malawi.

Katika mchezo huo kiungo wa Tanzania Mzamiru Yassin ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi (Man of the Match) baada kuonesha kiwango cha hali ya juu wakati wote wa mchezo huo.

Akizungumza na mwandishi wa Super Sport mara baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo, Mzamiru, aliitangaza vyema lugha ya Kiswahili baada ya kujibu maswali yote aliyokuwa akiulizwa kwa Kiswahili, kitendo hiko kimeonyesha kufurahishwa na mashabiki wengi wa soka ambao wamemuunga mkono.

Mchezaji Mzamiru Yassin akifanyiwa mahojiano na Mtangazaji wa Super Port

 

Ni mara ya pili mfululizo tuzo ya Man of the Match inachukuliwa na mchezaji wa kitanzania, mechi ya kwanza Shiza Kichuya alitangazwa mchezaji bora wa mechi waliyocheza dhidi Malawi ambapo mchezaji huyo aliifungia Stars magoli mawili yaliyoipa ushindi.

Naye golikipa Aishi Manula alifanya kazi ya ziada ya kuokoa mpira wa kona dakika ya sita tu tangu kuanza kwa mchezo wakati Angola walipokuwa wakitafuta goli la dakika za mapema.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents