Starz Kuandika Historia Mpya

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera amewataka wachezaji wa Taifa Stars wahakikishe wanaandika upya hishoria katika soka kwa kuibwaga Sudan na kufuzu kwa fainali za Afrika.

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera amewataka wachezaji wa Taifa Stars wahakikishe wanaandika upya hishoria katika soka kwa kuibwaga Sudan na kufuzu kwa fainali za Afrika.


Bendera ambaye pia, ni kiongozi wa msafara wa timu hiyo ambayo inaondoka leo kwenda Sudan kwa ajili ya mechi ya marudiano alisema Stars ina kila sababu ya kushinda mechi hiyo kwa kuwa walionyesha uwezo mkubwa katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan iliyochezwa Dar es Salaam.


"Kwa sasa hatutaki visingizio upendeleo dhidi ya Sudan, mnachotakiwa kufanya ni kuhakikisha mnacheza kufa na kupona ili kuitoa timu hiyo muweze kufuzu kwa fainali za kwanza zitakazofanyika Ivory Coast," alieleza.


Alisema: "Stars inaye leo Leopold Tasso Mukebezi (meneja), Leodegar Tenga (Rais TFF) waliokuwa mabeki, mimi (Bendera) nikiwa kocha, leo bado tupo Stars ya sasa, tunataka kuiandika upya historia iliyodumu kwa miaka 28 baada ya kuipeleka Stars fainali za Afrika nchini Nigeria mwaka 1980."


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhammed Seif Khatib alisema wachezaji wajue kuwa wanaenda kwenye vita na lazima washinde kwani uwezo, nia na sababu wanazo za kufanya hivyo.


” Mimi naamini hiyo mechi Stars itashinda natamka kwamba tutashinda kwani hata kabla ya mechi ya awali nilisema tutashinda na tumeshinda kwa sababu uwezo tunao,” alisema.


Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Taifa ( BMT), Kanali Idd Kipingu aliwataka wachezaji wasiogope kwa kuwa wapo ugenini wakishambulia nao washambulie kwani kwa sasa walipofika ni kama kombania ya mbele kivita.


”Nimeota Stars wameshinda katika mechi hiyo na tumesonga mbele, na ndoto yangu ni yakinifu na tulichokiona hapa wiki mbili zilizopita tunataka iwe ni mara mbili ya hapo” alisema.


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF), Leodegar Tenga alisema hakuna jambo jema ambalo litamfariji akiwa rais wa TFF, kama Stars itashinda Jumamosi katika mechi yao ya marudio.


Kocha Marcio Maximo alisema kuwa Sudan wanafahamu ugumu wa mchezo huo, lakini alieleza kuwa watacheza mpira wa kushambulia ili kuhakikisha wanapata ushindi mapema.


Wakati huo huo, mwenyekiti kuu wa bodi ya Serengeti Breweries (SBL), Jaji Mark Bomani alikabidhi hundi ya Shilingi milioni 33 kwa Stars ikiwa ni ahadi yao ya kutoa shilingi milioni moja kwa kila mchezaji endapo wangeishinda Sudan.


SBL, pia ilikabidhi vifaa mbalimbali kwa Stars vikiwemo T-Shirt, track suit na viatu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents