Michezo

Stephan Kingue aongeza mkataba Azam FC

Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, umefikia makubaliano ya kumwongeza mkataba wa mwaka mmoja kiungo mkabaji raia wa Cameroon, Stephan Kingue.

 

Akithibitisha nyongeza hiyo ya mkataba mbele ya waandishi wa habari leo mchana, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema kuwa wamefikia uamuzi huo kufuatia mapendekezo ya Kocha Mkuu Aristica Cioaba, ambaye anataka kuendelea na huduma yake.

“Uongozi wa juu wa Azam FC ulikuwa na mazungumzo na mchezaji Stephan Kingue Mpondo, amekuwa na timu kwa kipindi cha mwaka mmoja hivi sasa mkataba wake umekwisha na mazungumzo yalikuwa juzi na jana, lakini tunashukuru Mungu ni kwamba Stephan Mpondo kwa mujibu wa taarifa ya mwalimu Cioaba bado anamuhitaji kikosini.”Amesema Idd

Jaffar Idd ameongeza “Hivyo uongozi umechukua jukumu la kuongea na mchezaji huyu na ninavyoongea na ninyi ni kuwa Mpondo atandelea kuwepo ndani ya Azam FC baada ya jana kukubaliana na uongozi na amepewa mkataba wa mwaka mmoja zaidi kwa maana ya kuendelea ndani ya timu yetu, ni mchezaji ambaye mwalimu amemkubali kwa maana ni mchezaji kiongozi uwanjani lakini moja ya sifa yake Mpondo ni nidhamu na kujituma zaidi uwanjani.”

Kiungo huyo aliyejiunga na Azam FC mwezi Novemba mwaka jana anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa ukabaji pamoja na kupiga pasi zinazofika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents