Burudani

Stereo asema mwaka huu ataachia ngoma 3 ,kuanza na ‘Usione Hatari’ ft Ben Pol

Rapper Stereo amesema mwaka huu ataachia hits 3 akianza na wimbo ‘Usione Hatari’ baada ya mwaka jana kubanwa na masomo na kushindwa kufanya vizuri.

Stereo

Stereo ambaye mwaka huu anahitimu Bachelor of science in urban and regional planning ameiambia Bongo5 kuwa mwaka jana alishindwa kufanya poa kutokana na kujikita zaidi kwenye masomo,hivyo mwaka huu ataachia hits song 3 akianza na ‘Usione Hatari’.

“Mpango wangu kwa mwaka huu ni kuangamiza,nitatoa hits song 3 ambapo ni kali Hata kama zitazidi lakini mwaka huu nitakuwa na hits song 3 au zaidi. Kwanza mwaka huu nafungua na wimbo wangu mpya ‘Usione Hatari’ambao nimemshirikisha Ben Pol, prodyuza ni DX kutoka noizmekaH na utatoka January 9 mwaka huu,” amesema Stereo.

Katika hatua nyingine Stereo amesema ingawa anafanya muziki kama sehemu yake ya maisha pia akihitimu masomo yake anatamani kuja kuwa mkurugenzi wa kampuni fulani.

“Baada ya kuhitimu masomo napenda nije kuwa msimamizi wa kampuni au mtawala ambae nitakuwa nawasimamia watu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents