Steve Nyerere afunguka baada ya kutoswa kwenye kamati ya mazishi ya Mzee Majuto ‘hawajanivunja moyo’ (+video)

Muigizaji Steve Nyerere ambaye amezoeleka kuwa mbele kwenye matukio makubwa ya misiba ya watu maarufu, hatimaye amefunguka baada ya jana kutotajwa kwenye kamati ya mazishi ya Mzee Majuto.

Steve Nyerere amesema kuwa licha ya kutokupangwa kwenye kamati hiyo lakini hajafa moyo na kwa sasa anawaomba wasanii wote waungane ili kuweza kuuziba salama mwili wa King Majuto.

Jana usiku Kamati ya Msiba iliundwa na Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (TDFAA) na Chama cha Waigizaji Taifa ambapo jina la Steve Nyerere lilipigwa chini hii ni kutokana na kukosa sifa ya moja kwa moja ya kutokuwa mwanachama wa TDFAA.

 

 

Related Articles

6 Comments

Bongo5

FREE
VIEW