Steve Nyerere awaasa wasanii wenzie kuwa na desturi ya kuwakumbuka wenzao waliofariki

Steve Nyerere akitia ubani kwenye shughuli ya kumuombea dua marehemu mwanae

Muigizaji wa filamu na mchekeshaji nchini Steve Nyerere amewataka wasanii wenzie kuwa na desturi ya kuwakumbuka kwa sala wasanii mbalimbali waliotangulia mbele za haki.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni katika dua aliyoiandaa kwaajili ya kumuombea dua mwanae, Steve amesema anasikia uchungu kuona wasanii hao wamesahaulika.

“Kwa mfano marehemu Max toka amefariki hakuna mtu aliyewahi kumkumbuka kumsomea dua, toka amefariki hakuna mtu aliyewahi kumsomea dua,kumwomba mwenyezi Mungu kwamba ampokee marehemu Max,” alisema Steve.

“Max alikuwa muhimu, kioo cha watanzania, leo ukimfufua Max ukamweka kwenye TV Tanzania nzima itakaa attention, lakini ya mwenyezi Mungu akipangilia basi tunamshukuru, mimi nikaona kwa fadhila zangu nikaamua nisome dua, nikakaa na madirector wangu nikaona tusome dua kwa Max lakini sio wasanii wa filamu tu kwasababu kuna wakina Steve 2K, Leila Khatibu, akina Nasma Hamisi Kidogo ,akina Jonh Mjema, wako wapi akina Dandu, Complex. Leo Complex kijana mdogo hatuko naye tena, kwahiyo nikaja kuthubutu nikasema kwamba pamoja na umaarufu wangu lakini maisha yana mwisho kwanini nisisome dua, kwanini nisimkumbuke Mungu?”

Baadhi ya waigizaji wenzake waliohudhuria shughuli hiyo

Kwa upande mwingine Steve alisema kuwa hivi karibuni ataachia filamu yake iitwayo Get Out na baadaye kutoa nyingine iitwayo Goodbye Mr President ambayo itazungumzia maisha ya rais Jakaya Kikwete.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents