Burudani

Steve Nyerere: Nimeanzisha kundi la watu wenye akili

Baada ya kutoonekana katika maandamano ya kupinga filamu za nje, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameamua kuweka wazi juu ya  kundi jipya alilolianzisha.

Steve ameeleza kuwa “niliamua kujitenga na baadhi ya wasanii wenzangu wa Bongo Muvi kwa sababu siwezi kukaa nao ndiyo maana nimeamua kuanzisha kundi langu la watu wenye akili wanaoweza kufanya mambo ya maana na kuleta mafanikio”.

Mchekeshaji huyo alizungumza maneno hayo na gazeti la Wikienda, na kusisitiza kuwa angeendelea kujumuika na waigizaji hao basi angekuwa mjinga kama wao.

“Kwanza mimi ndiye maarufu kuliko wao maana nina kipaji cha kuzaliwa, lakini wao wamejifunza, maisha yangu ni mazuri tofauti na wao ambao hata milioni tatu kwao kupata ni shida,” amesema Steve.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents