Burudani

Steve RnB azungumzia mipango ya ndoa na kwanini hawezi kuacha kufanya R&B

Hitmaker wa Jambo Jambo, Steven William a.k.a Steve RnB anatarajia kutangaza ndoa na mpenzi wake aliyemvisha pete mwezi Novemba mwaka jana, mara baada ya kumaliza ziara yake nchini Marekani.

224520_286538224781509_1370390326_n

“Ni kweli tunapendana, soon soon nitatangaza ndoa, baada ya safari yangu ya Marekani mwezi huu Machi nahisi itakuwa mapema tu baada ya kutoka huko,”Steve alikiambia kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM. Kwa upande mwingine, muimbaji huyo amesema ataendelea kufanya RnB, kwani ndio imemfanya awe Steve RnB na kujitofautisha na wasanii wengine.

“RnB ni kitu ninachokipenda, najisikia niko comfortable, napofanya naenjoy na kuburudika anytime ndio maana huwa nafanya kitu ambacho mashabiki wanakipenda. Kwahiyo hata wimbo unapofika kwa mashabiki unakuwa wa aina yake nakuonekana mimi wa tofauti sipendi kufanya kama watu wengine wanavyofanya kwa kukimbilia kuimba afro pop.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents