Michezo

Steven Gerrard arudi Liverpool kujiweka fiti zaidi

Nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard amerudi katika mji wake wa nyumbani kufanya mazoezi na timu yake ya zamani tangu umalizike msimu wa Major League Soccer na timu ya LA Galaxy ya Marekani. Amekaribishwa na kocha Jurgen Klopp siku ya Jumatatu.

gerrard1
Steven Gerrard akielekea Melwood, Liverpool kufanya mazoezi

Mjerumani huyo amefanikiwa kumaliza mazungumzo haraka kuhusu kumrudisha Gerrard Anfield – kwani anarudi klabuni kufanya mazoezi.

klopp
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp akiwasili katika uwanja wa mazoezi mjini Liverpool

“Nilizungumza na Steven, kwa simu na kwa meseji,” alisema Klopp kabla ya ushindi na Rubin Kazan katika ligi ya Ulaya mwanzoni wa Novemba.

“Ni gwiji wa Liverpool, bila shaka. Lakini mkataba wake, najua kwa sasa uko Marekani.”

“Lakini kwa likizo hii, nilimwambia. “Unaweza kuja muda wowote unaotaka; unaweza fanya mazoezi na sisi, na kufanya lolote zuri kwa ajili yako. Milango iko wazi kwa ajili yako. Huo ndio ukweli.

“Lakini hakuna la ziada. Kila mtu anaweza kujifunza kutoka kwa Stevie, lakini najaribu kuelewa.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents