Michezo

Steven Gerrard astaafu kuichezea timu ya taifa ya England

Nahodha wa England na club ya Liverpool, Steven Gerrard hatimaye ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa lake la England akiwa na miaka 34.

steven-gerrard-2014-celebration-goal

Gerrard amejiimarisha kwenye kikosi cha Uingereza tangu mwaka 2000 walipoipiga Ukraine kwa mabao mawili kwa nunge. Kiungo huyo wa Liverpool amesema aliufurahia muda wote alipoichezea timu ya taifa na kwa kweli ni siku ya masikitiko kwake.

Hivi sasa Gerrard atakuwa katika nafasi za juu za ubalozi katika chama cha soka cha England. Anastaafu akiwa amecheza michuano mikubwa sita na kufunga mabao 21. Na hivyo kushika nafasi ya tatu baada ya Peter Shilton na David Beckham.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents